Siku ya Jana timu ya Simba Sc ilikuwa Mtwara ikicheza dhidi ya Namungo na japo ilishinda goli tatu kwa moja dakika za mwishoni kabisa, ilimkosa mchezaji wake Clatous Chama ambaye alisafiri kwenda Kitwe Zambia baada ya taarifa za kifo cha mke wake.
“Uongozi wa Klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mke wa kiungo wetu Clatous Chama (@realclatouschama), Mercy Mukuka uliotokea leo asubuhi nchini Zambia.
Timu inaungana na familia ya Chama katika kipindi hiki kigumu. Tunawaombea Mungu awape subira wote walioguswa na msiba huu katika muda wote wa maombolezo.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.”
Licha ya hilo, wachezaji mbalimbali wa Simba pia walitoa rambirambi zao pia kwa mchezaji huyo huku Manara akidai kuwa tmu itatuma watu maalum kwa ajili ya kushirikiana na Chama katika kipindi hichi kigumu!
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Pole sana Chama