Kocha wa klabu ya Inter Milan Simeone Inzaghi raia wa kimataifa wa Italia ameweka wazi kua ana furaha ya kuendelea kusalia kwa wababe hao wa soka kutoka nchini Italia.
Kumekua na taarifa mbalimbali zikimuhusisha kocha Inzaghi na na vilabu mbalimbali barani ikisemekana ataondoka ndani ya timu hiyo,Lakini kocha huyo amekanusha taarifa hizo na kusema ana furaha ndani ya Inter Milan.Kocha huyo wa zamani wa Lazio amekua na wakati mzuri sana ndani ya kikosi cha Inter Milan huku akiipeleka fainali ya michuano ya ulaya msimu ulioisha,Ikiwa ndio sababu za vilabu mbalimbali kuvutiwa na ubora wa kocha huyo.
Klabu ya Manchester United wanatajwa zaidi kuvutiwa na kocha huyo wakiona ni mtu sahihi wa kurithi nafasi ya kocha wasasa wa klabu hiyo Erik Ten Hag ambaye hafanyi vizuri kwasasa, Lakini kocha huyo ameeleza wazi kua bado ana furaha ndani ya viunga vya San Siro.Kocha Simeone Inzaghi ameyazungumza hayo jana baada ya mchezo wa ligi kuu ya Italia dhidi ya klabu ya Atalanta ambapo walipata ushindi wa mabao manne kwa bila, Ndipo kocha huyo alipotanabaisha kua anasikia tetesi za yeye kuondoka klabuni hapo lakini yeye ana furaha ndani ya timu hiyo.