Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva anayekipiga katika klabu ya Al Qadisiya inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Saudi Arabia amefungua mlango wa magoli baada ya kufunga goli kwenye mechi ya kwanza ya msimu mpya wa ligi hiyo.

MSUVA, Simon Msuva: Afungua Mlango wa Mabao., Meridianbet

Msuva aliipatia timu yake goli la kusawazisha mnamo dakika ya 60 na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-1 ambao mechi iliisha kwa timu yake kupoteza kwa 3-1 dhidi ya Al Akhdoud ambao wapo kileleni mwa msimamo wa ligi daraja la kwanza ya Saudi Arabia.

MSUVA, Simon Msuva: Afungua Mlango wa Mabao., Meridianbet

View this post on Instagram

 

A post shared by Simon Msuva (@smsuva27)

Msuva amesajiliwa na timu hiyo baada ya kushinda kesi yake na waajiri wake wa zamani ambao ni mabingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika CAFCL ambao walifikishana kwenye mahakama ya FIFA kudai malipo yake ya mshahara na posho zingine.

katika kikosi hicho yumo pia aliyekuwa mshambuliaji wa Al Ahly ya Misri Walter Bwalya ambaye nae alitemwa na miamba hiyo ya Misri.

MSUVA, Simon Msuva: Afungua Mlango wa Mabao., Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa