Mahusiano kati ya mwalimu wa klabu ya Real Madrid aliyepata mkataba mnono wa kuwafunza kwa awamu ya pili baada ya wengine kuonekana wanashindwa kabisa kuendana na falsafa za klabu hiyo na malengo yanayohitajika yamekuwa na sintofahamu kati ya Zidane ambaye ni kocha na Bale ambaye ni nyota mkongwe ndani ya klabu hiyo.
Kwa hali ilivyo uwepo wa Bale hauna tija yoyote mbele ya Zidane kwa sasa ambaye anaangalia namna ya kukijenga kikosi chake hicho ili kufuta aibu na machozi ya mashabiki ambao wameugulia msimu mzima.
Mwezi ujao atakuwa anatimiza miama 30 na kwa hatua hiyo ni vigumu sana kwa klabu nyingine zenye nia naye kulipa mshahara wa €18m kama atasajiliwa na klabu yoyote ile. Jambo hilo linaweza kuwa gumu kutokana na umri wa nyota huyo kusogea sana kwa sasa na hata nafasi yake kuonekana uwanjani imekuwa finyu sana.
Zidane ameweka wazi kwenye mechi yake dhidi ya Real Betis baada ya kupoteza 2-0 kwamba hata angepewa nafasi ya kubadili wachezaji wanne kwenye mchezo ule asingeweza kumpa Bale nafasi ndani ya kikosi chake. Hiyo ni dalili ya mwanzo kabisa kwamba haoni uhitaji wa kuwa naye kikosini hapo kwa sasa.
Kama huu utakuwa ni mwisho wa Bale kwa hakika sio mwisho mzuri kwenye maisha yake ya soka hasa ikiangaliwa mchango alioutoa kikosini hapo hasa kwa klabu hiyo kwa kuipa mataji yakiwepo yale ya klabu bingwa barani Ulaya, makombe ya ligi na kuifungia klabu hiyo zaidi ya magoli 100. Pia, akikumbukwa kwa magoli yake ya ushindi kwenye mechi muhimu.
Zidane, ambaye aliondoka klabuni hapo mara baada ya kutwaa ubingwa wa klabu bingwa, hana historia ya kumpa uhalisia wa kile anachokifanya nyota hiyo kiwe kizuri au hata kikiwa na manufaa kwa klabu. Jambo hilo liliwahi kuzungumziwa na Bale mwenyewe kwamba hana historia ya kupongezwa hata anapofanya vizuri na hata alipowapa ushindi mbele ya Liverpool hakupewa alama kwa tukio lile.
Hadi sasa amecheza mechi 12 pekee ndani ya ligi hiyo huku nyingi akiwa hajapata nafasi ya kumaliza dakika zote. Wamemaliza ligi hiyo wakiwa nyuma kwa alama 19 kutoka kwa vinara wa ligi hiyo, Barcelona na wakiwa hawajashinda mechi zao tatu za mwisho.
Wengi walihisi atakuwa mbadala wa Ronaldo lakini haijatokea kabisa. Zidane anataka watu kama Paul Pogba, Luka Jovic, Eden Hazard ndani ya kikosi chake.
Povel
Duh