SINGIDA BLACK STARS KUSHUSHA KOCHA MPYA

Siku chache zilizopita klabu ya Singida Black Stars iliwasimamisha kazi Kocha Mkuu Patrick aussems na msaidizi wake Denis Kitambi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni matokeo yasiyoridhisha.

Baada ya sakata hilo la kusimaishwa kazi bodi ya wakurugenzi ya Klabu hiyo ikawakabidhi timu Ramadhan Nswanzirumo na Muhibu Kanu kukaimu nafasi za waliosimamishwa mpaka pale watakapotoa taarifa nyingine.

Leo Singida Black Stars wamemtambulisha David ouma kama kocha msaidizi mpya wa klabu hiyo ambaye moja kwa moja anaenda kuwa pamoja na Nswanzirumo na Kanu ambao tayari wameiongoza klabu katika mchezo mmoja dhidi ya Azam Novemba 28,2025 ambao wamepoteza kwa mabao 2-1.

Ouma alikuwa kocha mkuu wa Coastal Union msimu uliopita lakini mwanzoni mwa msimu huu aliondoshwa kufuatia matokeo yasiyoridhisha klabuni hapo.

Acha ujumbe