Sintofahamu Hatma ya Ramos Madrid

Sergio Ramos na Real Madrid bado hawajakamilisha mazungmzo juu ya mkataba mpya wa nahodha huyu wa Los Blancos, lakini wakala wake anasisitiza hakuna sababu ya mtu yeyote kuwa na wasiwasi.

Ramos alijiunga na Madrid mnamo 2005 kutoka Sevilla na ameendelea kuwa muhimu sana kwa kilabu, amecheza karibu mechi 650 na kushinda tuzo nyingi.

Sasa akiwa na miaka 34, Mhispania huyu ni kama ana ukaribia usiku katika majukumu yake ya soka, lakini akiwa ameichezea Madrid mechi 25 kati ya 27 kwenye LaLiga kabla ya coronavirus, bado anaonekana kuwa mchezaji muhimu kwa Zinedine Zidane.

Mkataba wa Ramos unamalizika baada ya mwaka mmoja, na kuna maoni kuwa hatma yake ya muda mrefu pengine inaweza kuwa rehani ikiwa Madrid wataamua kutokuongeza mkataba wao.

Lakini wakala wa Ramos, ambaye ni kaka yake Rene, anaamini pande zote mbili zinataka nyota huyu astaafu soka akiwa Santiago Bernabeu.

“Soka linazunguka sana lakini kuna nia nzuri kwa pande zote mbili,” wakala huyo aliiambia Radio Marca.

“Natumaini atastaafu kwenye Real Madrid, ni ndoto yake na ninaelewa kuwa itakuwa nia ya kilabu pia.”

“Mpaka leo, hatujazungumza juu ya kitu chochote lakini hakuna haja ya kushtushwa. Wakati klabu itakapofikiria, tutaanza kuongea.”

Kwa maana hii, Sergio Ramos analazimika kusubiri maamuzi ya klabu ikiwa wataamua kumuongezea mkataba au lah! lakini matarajio makubwa ni kuwa atapata mkataba mpya.

37 Komentara

    Madrid hawako tayari kumpoteza ramos japo ana umri mkubwa lakini ni mtu muhimu sana pale bernabeu

    Jibu

    Kama vipi astafuu tu aendelee kuweka heshima

    Jibu

    Hatima ya mwisho ni kumsikiliza wakala wake yeye ndo ambaye anaeyemtafutia mchongo Kama mpaka anaongea na radio marca hivyo Kuna habari huenda akabaki kumalizia msimu wake akiwa wote akiwa Madrid

    Jibu

    Hatoki jeshi.

    Jibu

    Ramos Bado Sana real Madrid

    Jibu

    Madrid wanamkubali sna Ramos japo anaumri mkubwa lakini bado yupo vizuri.

    Jibu

    Kama vip astaafu aendelee kuweka heshima

    Jibu

    Wampe tu mkataba mpya bado yupo vizuri

    Jibu

    Ramos Bado yuko vizuri wampe tu mkataba

    Jibu

    Yupo vizuri sanaa

    Jibu

    Ramos yupo vizuri! Me naona akatafute changamoto nyingine#meridianbettz

    Jibu

    Ramos bdo yuko vizur aende Juve kwa wahenga wenzie

    Jibu

    Ntafurahi endapo atabaki kuwepo Real Madrid maan ukitaja Madrid lazima umtaje Ramos

    Jibu

    Ramos bora abaki

    Jibu

    akuna real bila Ramos na hakuna Ramos bila real Madrid💪💪💪

    Jibu

    Mkataba wake ukiisha astaafu tu

    Jibu

    gud newz asante

    Jibu

    Ila anakaa kwa wasi wasi sana #Meridianbettz

    Jibu

    Ramos jipemoyo ww mtu mkubwa usikae kwasiwasi Madrid bado upo jembe waho

    Jibu

    Huyo mshikaji jembe

    Jibu

    Madrid hawawezi kumuachia Ramos ingawa umri umeenda

    Jibu

    Tuwaachie viongozi wake#meridianbetz

    Jibu

    Ramos abaki Real Madrid

    Jibu

    Yuko vizur sana

    Jibu

    Habari mjema

    Jibu

    Ramos yupo vizuri

    Jibu

    Madrid cjui wanakwama wap mbona mshikaji yuko vizuri sana

    Jibu

    Ramos bado wamo na anahitajika kuendelea kutoa mchango Santiago lakini pia Club inatakiwa kuandaa warithi wa nguli huyu anayezeeka na utamu wake#meridianbettz

    Jibu

    Hatima ya mwisho ni kumsikiliza wakala wake yeye ndo ambaye anaeyemtafutia mchongo#meridianbettz

    Jibu

    Duh

    Jibu

    Ramos wampe tu kandarasi mpya

    Jibu

    Yuko vizuri Ramos ila umri umeenda apumzike tu

    Jibu

    Ramos anastahili kumalizia soka lake pale na tena anastahili Heshima kwa kujitoa kwake juu ya Madrid.

    Jibu

    Ramso talent player

    Jibu

    Ramos jeshi awezi kutoka

    Jibu

    Madrid wanaanzaje kumpoteza kiungo muhimu na mahili kama Ramos

    Jibu

    Abaki tuu asiondoke

    Jibu

Acha ujumbe