Sir Jim Hana mpango wa Kumnunua Mbappe

Bosi mpya wa klabu ya Manchester United Sir Jim Ratcliffe ameweka wazi kua hana mpango wowote wa kumnunua mshambuiliaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya PSG Kylian Mbappe.

Sir Jim ameyazungumza hayo wakati akifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari ambapo walimuuliza kama anavutiwa na kumnunua mshambuliaji Mbappe na yeye akisema”Ningejaribu kutafuta Mbappe anayefuata kuliko kutumia pesa nyingi kununua mafanikio, Sio ujanja sana kumsajili Mbappe kwasasa, Ni changamoto zaidi kupata Mbappe anayefuata, Bellingham anayefuata, au Roy Keane anayefuata”sir jimMshambuliaji Kylian Mbappe ametangaza kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu na vilabu kadhaa vinahusishwa na kupata saini yake, Lakini bosi huyo wa klabu ya Man United amekanusha kuhitaji saini ya staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Bosi huyo anaona sio jambo la busara kutoa pesa nyingi kwasasa kumsajili Mbappe zaidi yeye anafikiria namna atakavyoweza kumpata Mbappe mwingine, Hii ikimaanisha mipango yao ni kupata mchezaji mwenye ubora kama wa Mbappe lakini akiwa na umri mdogo.sir jimKutokana na taarifa kutoka kwa bosi Sir Jim Ratcliffe ni wazi Man United haina mpango wowote wa kuingia kwenye vita ya kumuwania Kylian Mbappe pale tu atakapokua huru kwenye majira ya joto mwezi wa sita baada ya ligi kumalizika.

Acha ujumbe