Kiungo wa zamani wa Liverpool na PSG Mohamed Sissoko amedai kuwa mshambuliaji wa Psg, Kylian Mbappe na Erling Haaland wa Manchester City wanaweza kufikia viwango vya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Ambapo mchezaji huyo wa PSG Mbappe na mshambuliaji wa Manchester City Haaland wamethibitisha kuwa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu na rekodi za kufunga mabao katika misimu ya hivi karibuni zikizidi kuvutia wapenzi wa soka Duniani.
Haaland alifunga mabao 67 katika misimu yake miwili na nusu kwenye Bundesliga akiwa na Borussia Dortmund, na baadaye alihamia Ligi Kuu ya Uingereza katika klabu ya City ambapo ameweza kufunga mabao 14 katika mechi 10 za nje katika mashindano yote kwenye kikosi cha Pep Guardiola.
Wakati huo huo, Mshindi Kombe la Dunia mwaka 2018 na timu ya PSG Mbappe hajaona shida nae kufunga mabao kwa miaka kadhaa na sasa yupo kwenye hatua kubwa zaidi. Huku Messi na Ronaldo wakikaribia mwisho wa maisha yao kwenye soka, maswali juu ya nani atachukua nafasi yao bila shaka yameibuka, Ambapo;
Sissoko anaamini Mbappe na Haaland wanaweza kufikia viwango hivyo, akiiambia Stats Perform: “Wanafunga mabao mengi. Ni wachezaji tofauti pia”.
“Nadhani Mbappe ni mchezaji wa juu, Haaland pia. Nadhani wanaweza kuwafikia Cristiano Ronaldo na Messi, kwa hakika.”