Skriniar Ajiunga na PSG Huku Kocha Mpya Luis Enrique Akianza kazi

Milan Skriniar amejiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa bure. Beki huyo wa kati wa Slovakia mwenye miaka 28, alimaliza muda wake wa miaka sita katika klabu ya Inter Milan wakati mkataba wake ulipokamilika mwezi uliopita.

 

Skriniar Ajiunga na PSG Huku Kocha Mpya Luis Enrique Akianza kazi

Sasa anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Luis Enrique tangu kutambulishwa kama mbadala wa Christophe Galtier jana.

Akisaini mkataba wa miaka mitano, Skriniar alisema: “Nina furaha sana kuwa sehemu ya klabu hii nzuri. PSG ni moja ya klabu bora zaidi duniani, yenye wachezaji wa kiwango cha juu na mashabiki wa ajabu.”

Skriniar alicheza mechi 246 akiwa na Inter akitokea Sampdoria mwaka 2017. Alishinda taji la Serie A akiwa na Nerazzurri mnamo 2020-21 huku akinyanyua Copa del Rey mara mbili.

Skriniar Ajiunga na PSG Huku Kocha Mpya Luis Enrique Akianza kazi

Mchezaji huyo wa kimataifa mwenye mechi 60 alianza kwa vijana wa Simone Inzaghi katika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, na kuishia kwenye timu iliyopoteza kwa Manchester City.

Ukiwa unaendelea kuwaza wapi utapata pesa kirahisi, Meridianbet wanakwambia wao ndio sehemu pekee kwa wewe kuwa bingwa. Je unasubiri nini kuingia www.meridianbet.co.tz na ucheze sasa.

Luis Enrique anataka kukijenga upya kikosi chake kufuatia kuachwa kwa Lionel Messi na Sergio Ramos mapema msimu huu wa joto.

Skriniar Ajiunga na PSG Huku Kocha Mpya Luis Enrique Akianza kazi

Mustakabali wa mshambuliaji nyota Kylian Mbappe bado hauko wazi, huku rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi akiwaambia wanahabari jana kuwa msimmao wake upo wazi sana na hataki kurudia kila wakati ikiwa Mbappe anataka kubaki, wanataka kubaki.

“Lakini anahitaji kusaini mkataba mpya. Hatutaki kumpoteza mchezaji bora zaidi duniani bila malipo, hataondoka bure, hivyo ikiwa atabadilisha mawazo yake leo, sio kosa langu. Hatutaki kumpoteza mchezaji bora wa dunia bure, hilo liko wazi.”

Acha ujumbe