Skudu Azunungumza Jambo

SKUDU Makudubela nyota wa Yanga ameweka wazi kuwa hana tatizo lolote na benchi la ufundi la timu hiyo linalonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga akitokea Marumo Gallants hajawa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba uliopo ndani ya timu hiyo.skuduMbali na ushindani pia alianza msimu akipambania hali yake baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga alipopata maumivu ya mguu dakika ya sita alipochezewa faulo na James Akamiko.

Nyota huyo amesema: “Nipo Yanga na nifurahi kuona tunapata matokeo kwenye mechi zetu ambazo tunacheza hilo ni jambo la msingi. Kutokucheza ama kucheza hilo halinipi shida kwani kuna wachezaji wengi ndani ya Yanga.skudu“Wanapofunga kwenye mechi zetu wale wanaopewa nafasi hii inatupa nguvu sisi kwa ajili ya kuendelea kupambania malengo yetu. Kuhusu nani aanze kwenye mchezo husika huo ni mpango wa benchi la ufundi na hatuna matatizo nao kabisa” Alisema Skudu Makudubela

Acha ujumbe