Baada ya maneno kuwa mengi kumuhusu Dean Henderson, kocha Ole Gunnar Solskjaer ameamua kuweka wazi kuhusu hatma ya mchezaji huyo ndani ya Man United.

Kwa wiki kadhaa zilizopita hasa wikiendi iliyopita, taarifa zilisambaa kwamba Henderson anatarajia kuondoka United kwa mkopo mwezi Januari kufuatia kukosa namba kwenye kikosi cha United.

Dean Henderson ameitumikia Manchester United mara 3 pekee kwenye msimu huu mpaka sasa. Mchezo wa mwisho, United walipoteza mbele ya Istanbul Basaksehir (2-1) Dean Henderson akiwa golini.

Solskjaer ametumia nafasi ya kuwazungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Istanbul Basaksehir kuzungmzia taarifa zilizosambaa kuhusu Henderson.

Solskjaer, Solskjaer Hanawasiwasi na Dean Henderson, Meridianbet
Dean Henderson Akiwa uwanjani kulinda goli la Man United

Ole amesema “Dean anataka kubaki na kuichezea Manchester United“. Akijibu swali la mwandishi ambaye aliuliza uwezekano wa Dean kucheza mchezo 1 pekee (dhidi ya Everton kwenye EFL Cup) kabla ya 2020 kuisha endapo hatacheza kwenye mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa.

Ole alijibu ” sioni uhalisia wa Dean kucheza mchezo mmoja kabla ya Krisimasi. Unajua tunamichezo mingapi? Kwa sababu hiyo, sikubaliani kabisa na mchezo wa leo kuwa wa maamuzi kumuhusu Dean.

“Ndio amerejea, anafanya vizuri kwenye mazoezi, amekuwa mtu mzima sasa. Kwa upande wangu, anafanya mazoezi na makipa bora duniani. Ana nafasi ya kuwa golikipa bora duniani.

“Ni ushindani mkubwa kati yao (magolikipa), kwahiyo siwezi kubabaishwa na maneno yenu kwamba hana nafasi.”

Pamoja na kuongelea suala la Dean Henderson, Ole Gunnar Solskjaer anatarajia kuipata huduma ya Paul Pogba kwenye mchezo dhidi ya Istanbul Basaksehir leo usiku. Hii ni baada ya kiungo huyo kurejea mazoezini. Pia, ameongeza kuwa Luke Shaw atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 6 baada ya kupata majeraha ya paja.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

23 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa