Solskjaer Yupo Tayari Kurudi Man United

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer na gwiji wa klabu hiyo amefunguka kua yupo tayari kurejea ndani ya klabu hiyo kama atatakiwa kufanya hivo na mabosi wa klabu hiyo.

Chombo kimoja cha habari kimefanya mazungumzo na Solskjaer na kumuuliza kama kocha huyo yupo tayari kurejea ndani ya viunga vya Old Trafford na kusema hapendi kuzungumzia kazi za makocha wengine, Lakini yupo tayari kurejea ndani ya Manchester United kama atapata nafasi hiyo.solskjaer“Sipendi kuzungumzia kazi za makocha wengine, lakini ndiyo.”

“Bila shaka, ningefanya hivyo!”

Kocha huyo aliondolewa ndani ya kikosi cha Manchester United mwaka 2021 na nafasi yake kuchukuliwa na Michael Carrick, Ralf Rangnick, na baadae Erk Ten Hag ambaye yupo mpaka sasa ndani ya timu hiyo, Lakini bado timu hiyo haijakaa sawa kama ambavyo inahitajika hivo inawezekana Solskjaer akarejea United kama Ten Hag ataondolewa kutokana na muenendo mbaya wa timu.

Acha ujumbe