Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hot Spurs Heung-min Son amemaliza ukame wake wa mabao kwenye ligi ya Premia kwa kufunga hattrick yake ya kwanza katika kipindi cha pili huku Tottenham Spurs ikiilaza Leicester City kwa mabao 6-2.

 

Son Apiga Hattrick Yake ya Kwanza

Mshambuliaji huyo wa Korea Kusini alikuwa anawekwa benchi na Antonio Conte kutokana na na kuwa na kiwango ambacho alianza nacho msimu huu ambapo alikaa benchi katika mchezo wake wa mwisho kabla ya mapumziko ya Kimataifa.

Lakini mshindi huyo wa kiatu cha Dhahabu msimu uliopita aliingia akitokea benchi baada ya mapumziko na kuukamata mchezo na kumfanya afunge mabao matatu ndani ya robo saa ya mchezo. Mabao yote matatu yalikuja kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo matokeo hayo yanazidi kumfanya kocha wa Leicester City Brendan Rodgers.

 

Son Apiga Hattrick Yake ya Kwanza

Son anakuwa ni mchezaji wa kwanza EPL kufunga hattrick kama mchezaji aliyetokea benchi na katika kipindi cha pili. Na baada ya matokeo hayo Conte na vijana wake wamepanda hadi nafasi ya pili ya msimamo wakiwa sawa na Manchester City kwa alama 17, huku wakisubiria matokeo ya leo ya Arsenal.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa