Son: Bado Nipo Sana Spurs

Winga wa klabu ya Tottenham Hotspurs Heung Ming Son raia wa kimataifa wa Korea Kusini amesema hana mpango wa kuondoka ndani ya klabu hiyo na kutimkia Uarabuni.

Winga Son ameyasema hayo baada ya kuhusishwa kuondoka ndani ya klabu hiyo na kwenda Uarabuni katika kipindi hichi cha usajili wa dirisha kubw, Lakini winga huyo amesisitiza kua bado ana mambo mengi ya kufanya katika ligi kuu ya Uingereza.sonTimu kutoka Saudia Arabia zimekua zikifanya usajili wa kushtua katika ligi mbalimbali barani ulaya, Winga huyo wa klabu ya Tottenham pia alikua anahusishwa na kujiunga na vilabu kutoka nchini Saudia lakini yeye mwenyewe ameknusha taarifa hizo.

Winga Son amesema pesa sio kila kitu kwake kwakua yeye anajivunia kucheza mpira haswa katika ligi pendwa kwa upande wake ndio kitu cha muhimu kwasasa na suala la yeye kujiunga na ligi ya Urabuni sio kipaumbele chake na matumaini yake ni kubaki Spurs.sonSon amekua mchezaji muhimu sana ndani ya kwa miaka kadhaa sasa kando ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Harry Kane, Winga huyo amekua na ubora wa hali ya juu pia ndani ya timu hiyo kitu kinachofanya awindwe na vilabu mbalimbali lakini suala la kwenda Uarabuni kwasababu ya pesa amelikanusha vikali.

Acha ujumbe