Southgate Amtema Jadon Sancho Uingereza.

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza, Gareth Southgate, ametangaza kikosi cha timu hiyo kitachoshiriki mashindano ya kimataifa mwezi huu.

Timu ya Taifa ya Uingereza, inajengwa na wachezaji wengi ambao ni vijana na wanachipukia kwenye ulimwengu wa soka. Uwepo wa wachezaji wenye viwango tofauti tofauti, kila mmoja katika ubora wake, ni miongoni mwa changamoto anazokutana nazo Southagate.

Kuelekea michezo ya kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia, Qatar 2022, Gareth Southgate ametoa orodha ya wachezaji atakaowatumia kwenye michezo ya timu za Taifa kuanzia wiki ijayo.

Kierran Trippier

Jadon Sancho, Mason Greenwood na Kierran Trippier ni miongoni mwa wachezaji nyota walioachwa kwenye kikosi cha Uingereza. Haijajulikana sababu zilizopelekea wachezaji hawa kuachwa lakini huenda nafasi zao kwenye vilabu walivyopo, zimewagharimu.

Sancho hajaonesha makali yake kwenye kikosi cha Manchester United tangu ajiunge na timu hiyo. Trippier amekuwa akisugua benchi kwa muda sasa kwenye kikosi cha Atletico Madrid. Greenwood amekuwa na msimu mzuri ndani ya United lakini sababu ya kutokuitwa kwake haijawekwa wazi.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza kilichotangazwa na Southgate hiki hapa:

Magolikipa: Sam Johnstone (West Bromwich Albion), Jordan Pickford (Everton), Aaron Ramsdale (Arsenal)
Walinzi: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Ben Chilwell (Chelsea), Conor Coady (Wolverhampton Wanderers), Reece James (Chelsea), Harry Maguire (Manchester United), Tyrone Mings (Aston Villa), Luke Shaw (Manchester United), John Stones (Manchester City), Kyle Walker (Manchester City)
Viungo: Jude Bellingham (Borussia Dortmund), Jordan Henderson (Liverpool), Mason Mount (Chelsea), Kalvin Phillips (Leeds United), Declan Rice (West Ham United), James Ward-Prowse (Southampton)
Washambuliaji: Tammy Abraham (AS Roma), Jack Grealish (Manchester City), Phil Foden (Manchester City), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Marcus Rashford (Manchester United), Bukayo Saka (Arsenal), Raheem Sterling (Manchester City)

MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA


Acha ujumbe