Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate amepingana na kauli ya mchezaji wake Phil Foden anayekipiga klabu ya Manchester City juu ya yeye kupendelea zaidi kucheza katikati.

Winga Foden aliweka wazi anapenda kucheza nafasi ya katikati lakini kocha Southgate wakati akifanya mahojiano alisema mchezaji huyo ni mzuri zaidi akitokea pembeni nafasi ambayo yeye anamchezesha.fodenMchezaji Phil Foden amekua akicheza katikati ndani ya klabu yake ya Manchester City mara chache, Hivo kocha huyo akiongea na waandishi wa habari alisema Foden hachezi kati akiwa kwenye klabu yake na huenda kuna sababu ya hilo.

Mashabiki wengi wanaamini kocha huyo anakosea kumchezesha Foden pembeni kwakua mchezaji huyo ana ubora wa kucheza nafasi ya katikakati ambayo mara kadhaa imeonekana ikikosa ubunifu kwenye timu ya taifa ya Uingereza.fodenKocha Southgate anasema watu wanaangalia tu timu inapokua na mpira lakini wanapaswa kuangalia pia timu inapokua haina mpira inaenda kwa mtiririko gani, Kutokana na kauli hii ni wazi Foden hachezi katikati kwakua kocha huyo anahitaji wachezaji watakaoweza kuweka presha kwenye mpira na kuzuia vizuri kwenye eneo la kati.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa