Southgate Hali Tete Uingereza

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate anapitia kipindi kigumu kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo wakimshutumu kua ameshindwa namna ya kuipangilia timu hiyo.

Southgate anaiongoza Uingereza kwenye michuano mikubwa kwa mara ya nne michuano ya Euro mara mbili na michuano ya kombe la dunia mara mbili, Ambpo hatua kubwa aliyofanikiwa kufika ni fainali Euro 2020 na nusu fainali kwenye kombe la dunia mwaka 2018.southgateKutokana na mwenendo huo mabosi wa shirikisho la soka la Uingereza waliamini kocha huyo anaweza kuifikisha mbali timu hiyo kutokana na vipaji ambavyo nchi hiyo inaendelea kuvitengeneza kila siku, Lakini mashabiki wa timu hiyo wameanza kuona alipoifikisha timu hiyo ndio mwisho na hamna mafanikio watayapata kupitia kwa kocha huyo.

Kocha Southgate anatupiwa maneno hata na baadhi ya wachambuzi wa soka na magwiji wa zamani timu hiyo mbali na mashabiki wa timu hiyo, Hii inatokana na namna anavyoichagua timu hiyo kuelekea kwenye mchezo husika huku akishutumiwa kuwapanga baadhi ya wachezaji kwenye zisizo zao wakati wenye uwezo wa kucheza nfasi hizo wakiwa benchi.southgateBaada ya sare ya mchezo wa jana dhidi ya Denmark kocha huyo amenyooshewa vidole kutokana na kumpanga beki wa Liverpool Trent Alexender Arnold katika nafasi ya kiungo katika mchezo wa pili mfululizo, Huku ikionekana hana uwezo wa kucheza nafasi hiyo wakati viungo kama Kobbie Mainoo, na Adam Wharton wakiwa kwenye benchi.

Acha ujumbe