Kocha mkuu wa England Gareth Southgate amesema kuwa yupo tayari kuendelea kuweka heshima yake katika uteuzi unaoendelea wa Harry Maguire, akisisitiza kwamba beki huyo wa Manchester United anasalia kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa England.

 

Southgate Kuhusu Maguire

Maguire amekuwa akiachwa kwenye benchi ambapo Manchester United ikishinda mara nne mfululizo wa Primia Ligi, baada ya kuanza vipigo vyao mfululizo wakati wa ufunguzi wa kampeni wa ligi kuu mwezi uliopita.

Beki huyo ameanza mechi moja  tuuh kati ya tano zilizopita za United katika michuano yote, 1-0 Ligi ya Uropa dhidi ya Real Sociedad na kusababisha ukosoaji wa uamuzi wa Southgate kumwita kwa mechi zilizosalia za Ligi ya Mataifa ya England.

Lakini akizungumza kabla ya mkutano wa England na Italia huko San Siro, ambao utafuatiwa na ziara huko Ujerumani siku ya Jumatatu, Southgate alisisitiza kuwa Maguire anasalia kuwa katikati ya mipango yake.

 

Southgate Kuhusu Maguire

“Sifa yoyote niliyonayo ninaiweka hapo”, Sothgate alisema, “Nadhani siku zote unapaswa kuungwa mkono uamuzi wako, na tunahisi ni mchezaji muhimu. “Ni wazi sio hali nzuri . Unataka wachezaji wako bora wacheze mara kwa mara ili wawe katika sehemu nzuri na kiakili.”

England wamepoteza mechi mbili pekee kati ya 26 zilizopita, zote dhidi ya Hungary katika mechi za ligi ya Mataifa ya Juni. Hata hivyo hawajashinda michezpo yao minne iliyopita ambapo ni muda mrefu zaidi tangu Juni 2014.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa