SOWAH ATAJWA KUJIUNGA YANGA

MKALI wa kucheka na nyavu ndani ya Singida Black Stars kwenye mechi za ligi Jonathan Sowah raia wa Ghana inaelezwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Yanga ambao wanahitaji kuipata saini yake.

Sowah ndani ya ligi amefunga mabao matatu akiwa na uzi anaingia kwenye orodha ya washambuliaji waliomtungua kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra kwenye mchezo wa ligi msimu wa 2024/25 akiwa katupia jumla ya mabao matatu.

Rekodi zinaonyesha kuwa bao la kwanza nyota huyo alifunga Februari 7 ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar walipotoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Liti.sowah

Bao la pili alifunga kwenye mchezo waka wa tatu kuanza kikosi cha kwanza ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania mchezo uliochezwa Uwanja wa Meja Isahmuyo ilikuwa ni Februari 13 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Tanzania 0-1 Singida Black Stars.

Kwenye mchezo huo ugenini alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya dakika 90 kwa kuwa bao hilo lilikuwa ni la ushindi kwa Singida Black Stars wakikomba pointi tatu mazima.

Sowah akipachika bao la tatu kwenye mchezo dhidi ya Yanga inayotajwa kuwa itamalizana naye dirisha dogo la usajili kwa kuinasa saini ya nyota huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia mguu wake wa kulia kwenye kucheka na nyavu.

Ni Februari 17 2025 dakika za jioni Sowah alimtungua Diarra akiwa ndani ya 18 kwa mguu wake wa kulia akitumia makosa ya kipa huyo kutema mpira uliopigwa na Edmund John akiwa nje kidogo ya 18.

Mwisho ubao ukasoma Yanga 2-1 Singida Black Stars likiwa ni bao la tatu kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Medeama raia wa Ghana

Ikumbukwe kwamba mchezo wake wa pili ilikuwa dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex kwenye mchezo huu alianza kikosi cha kwanza na alishuhudia Februari 10 2025 ikiwa chungu kwa ubao wa Uwanja wa KMC Complex kusoma KMC 2-0 Singida Black Stars.

Acha ujumbe