Kocha wa Napoli ya nchini Luciano Spaletti amesema anaamini nyota wake walio kwenye ubora mkubwa kwasasa Victor Osimhen na Khvicha Kvaratskhelia wataendela kuwasha moto kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa leo dhidi ya Frankfurt.
Nyota Khvicha Kvaratskhelia na Osimhen wamekua kwenye ubora mkubwa kwa siku za hivi karibuni na kuisaidia klabu ya Napoli kutokana na kiwango ambacho wamekua nacho, Kitu ambacho kimemfanya kocha Spalletti kuendelea kuamini nyota hao wataendelea kua bora zaidi.Klabu ya Napoli leo itakua nchini Ujerumani wakikaribishw ana klabu ya Franfurt katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa ulaya, Huku Napoli ambao ni vinara wa ligi kuu ya Italia maarufu jama Serie A wakipewa nafasi kubw kushinda mchezo huo kutokana na ubora ambao wamekua nao msimu huu.
Kocha Spalletti amesema licha ya Osimhen na Kvaratskhelia kua bado wachanga sana lakini wameweza kutuma ujumbe kwa dunia na kuonesha wao ni wachezaji wa aina gani, Hiyo inatokana na uwezo ambao wameonesha vilevile wamekua na ushirikiano mzuri sana katika safu ya ushambuliaji ya Napoli.Kocha Luciano Spalletti kwa upande mwingine hakuacha kumpa sifa kocha wa sasa wa klabu ya Franfurt Oliver Glasner ambaye amekua akifanya vizuri tangu achukue timu hiyo mwaka 2021, Kocha Luciano amesema anamjua Glasner na anamheshimu kwakua anafanya kazi nzuri ndani ya Frankfurt.