Hakika kutokata tamaa ni silaha kubwa katika kuyafikia mafanikio. Baada ya ukame wa miaka 19, Sporting Lisbon wameibuka kidedea msimu huu.
Kunako Ligi Kuu soka nchini Ureno, klabu ya Lisbon ambayo imetoa mastaa kama Cristiano Ronaldo, Luis Nani na Bruno Fernandez, imevunja utawala wa Benfica na FC Porto uliodumu kwa miaka 19 kwenye historia ya Primeira Liga.
Sporting CP wametwaa ubingwa wa Ligi hiyo baada ya kuwafunga Boavista kwa goli 1-0. Goli pekee lililofungwa na Paulinho, limeifanya timu hiyo kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi 8 dhidi ya FC Porto wanaoshika nafasi ya pili zikiwa zimesalia mechi 2 msimu kumalizika.
Klabu hii inabeba ubingwa wa Primeira Liga ikiwa haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa. Huu ni muendelezo wa mafanikio ya klabu hiyo ambayo mapema mwezi Januari mwaka huu, Sporting Lisbon walibeba Kombe la Ligi.
Ni miaka mitatu tu imepita tangu mashabiki wa klabu hii wavamie uwanja na kuzua tafrani kwa wachezaji na wafanyakazi wa timu hiyo. Tukio hili lilipelekea kocha wa wakati ule (Jorge Jesus), baadhi ya viongozi wakubwa pamoja na raisi Bruno de Carvalho wote kujiuzulu nafasi zao.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Wamejitahidi sana
Hongereni sana mmefanya vizuri#meridianbett
Wamefanga vizur
Kidogo wanajitahidi ila waongeze juhudi
Hongera yao
Waendelee na moto huo huo
Hongera yao