Tottenham Hotspur inaripotiwa kuwa kwenye mpango wa kumuuza Dele Alli msimu huu wa joto, licha ya kiungo huyo kuanza michezo yao mitano ya mwisho ya msimu.

Mchezaji huyo wa miaka 25 alirejea kwenye kikosi cha kwanza chini ya Ryan Mason kufuatia wakati mgumu chini ya bosi wa zamani Jose Mourinho.

Hata hivyo, Dele Alli alihusika moja kwa moja katika goli moja tu katika kuanza kwake kampeni – akisaidiwa na Son Heung-min kwenye mechi waliyopoteza kwa 3-1 dhidi ya Leeds United.

Kulingana wa Football Insider, Spurs haikusudii kubadilisha uamuzi wao wa awali wa kutemana na nyota huyo wa kimataifa wa England kwenye dirisha lijalo la uhamisho msimu huu wa joto.

Spurs wanadaiwa kuwa walifanya uamuzi wa kumtumia Alli mara kwa mara mwishoni mwa 2020-21 kuonyesha talanta zake kwa wanunuzi, hivyo kimsingi yuko sokoni.

Alli amekuwepo Tottenham kwa misimu sita, akicheza jumla ya mechi 250 katika mashindano yote kwa upande huo wa London Kaskazini.


 

Bonasi ya 50% Kila Siku Katika Kasino za Evoplay hapa Meridianbet.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa