Jiji la London mambo ni moto. Harry Kane anawaumiza vichwa vigogo wa Tottenham Hot Spurs kuelekea usajili wa dirisha kubwa.

Baada ya kuendelea kukosa mataji akiwa na Spurs, Harry Kane anahusishwa na kuondoka klabuni hapo licha ya kuwa na mkataba wa miaka 3 na klabu hiyo.

Tottenham wameendelea kutaabika kwa misimu mingi licha ya kucheza fainali kadhaa kwa miaka ya hivi karibuni. Klabu hiyo iliamua kuwaondoa makocha wake – Mauricio Pochettino na Jose Mourinho licha ya makocha hao kuwaifikisha timu hiyo kwenye nafasi za kutwaa mataji bila mafanikio.

Bado Kane hajawasilisha maombi rasmi ya kutaka kuondoka Spurs wala hajazungumzia suala hilo na viongozi wa klabi hiyo. Lakini, inaaminika mshambuliaji huyo anahitaji kucheza kwenye klabu inayompatia nafasi ya kupambania makombe kila msimu. Hiki ni kitu ambacho hakipati akiwa na klabu hiyo.

Spurs, Spurs Hali Si Shwari, Kane Inakuaje Sasa?, Meridianbet
Daniel Levy

Japokuwa mmiliki wa Tottenham, Daniel Levy anajulikana kwa ugumu wake linapokuja suala la kufanya nae biashara. Hapa kuna mengi ya kuyaangalia. Kwanza, Levy anasakata kubwa la kuirudisha imani ya mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuingia kwenye mpango wa European Super League.

Pili, kuondolewa kwa Pochettino na Mourinho sambamba na madhara ya Covid19, ni dhahiri uchumi wa klabu umeathirika na hivyo kumuuza Kane ni fursa kwa klabu hiyo kutengeneza faida kubwa ambayo itawasaidia kujijenga upya.

Je, Harry Kane ataondoka Spurs au ataamua kuwa kama Fransico Totti na maisha yake ndani ya AS Roma?


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Spurs, Spurs Hali Si Shwari, Kane Inakuaje Sasa?, MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa