Spurs, Juventus, Inter na Atletico Wamtupia Jicho Mac Allister

Ripoti mbalimbali kutoka Fichajes zinasema kuwa klabu za Spurs, Juventus, Inter na Atletico zinamtupia Alexis Mac Allister wa Brighton na timu ya Taifa ya Argentina baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia katika Kombe la Dunia.

 

Spurs, Juventus, Inter na Atletico Wamtupia Jicho Mac Allister

Timu yake ilifuzu katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa mikwaju ya penalti dhidiya Uholanzi kufuatia sare ya 2-2 dakika 90 za mpira na kwenye mechi hiyo mwamuzi kuweka historia ya kutoa kadi za njano 18.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 ana kandarasi na Brighton hadi katikati ya 2025, akifunga mkataba mpya na Seagulls mwezi Oktoba na kumhakikishia kwa misimu miwili na nusu ijayo, na chaguo la nyongeza ya mwaka mmoja .

Spurs, Juventus, Inter na Atletico Wamtupia Jicho Mac Allister

Inter wanavutiwa zaidi, wakimtazama Mac Allister kama mbadala wa muda mrefu wa Marcelo Brozovic, wakati bosi wa Spurs Antonio Conte anataka kuongeza ubunifu kwenye safu yake ya kiungo.

Juventus imekuwa ikiwasaka wachezaji wengi kwenye Kombe la Dunia, huku Atletico wakiwa na hamu ya kuongeza ubora kwenye safu yao ya kiungo, huku Rodrigo de Paul akivutiwa pia.

Acha ujumbe