Nuno Espito Santo na Fabio Paratici wanahaha kunako soko la usajili kuelekea msimu ujao. Spurs wanahaha, nani anawafaa – nani hawafai?
Tottenham wapo sokoni kusaka wachezaji watakaoboresha kikosi cha timu hiyo kwenye baadhi ya nafasi. Kiungo na ulinzi ni maeneo ambayo Nuno na Paratici wanayatizama kwa jicho la kipekee.
Imeripotiwa kuwa Spurs inamvutia kasi kiungo wa AS Roma, Lorenzo Pellegrini. Roma kwa sasa ipo chini wa aliyekuwa kocha wa Tottenham – Jose Mourinho na itawapasa kutoa kitita cha takribani £26m ili waweze kumsajili mchezaji huyo. Hii ni thamani aliyowekewa Pellegrini kwenye mkataba wake na Roma.
Danny Ings amegoma kusaini mkataba mpya na Southampton na hivyo anaweza kuondoka majira haya au akasubiri msimu ujao uishe na aondoke kama mchezaji huru. Spurs wanamuona Ings kama mtu sahihi wa kusaidiana na Harry Kane kwenye safu ya mashambulizi.
Japokuwa, tetesi zinasema Southampton wanakuwa wagumu kufanya biashara hii na Spurs, hii ni kutokana na upinzani uliopo kati ya timu hizi na pengine ulianzia kwa Maurizio Pochettino ambaye alikuwa kocha wa Soton kabla ya kuwakimbia na kwenda Tottenham.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!
Ernest
Ngoja tuone