Taarifa zinaripoti kuwa meneja wa sasa wa Klabu ya Tottenham Hotspur, bwana Jose Mourinho ameweka wazi kuwa klabu yake haitafanya mambo mengi kwenye usajili wa Januari.
Spurs wameshinda mechi 5 katika mechi zao 8 za michuano yote walizocheza tangia Jose Mourinho achukue nafasi ya Mauricio Pochettino mwezi uliopita.
Kuna taarifa kuwa klabu hiyo inahitaji kuboresha kikosi chake kupitia usajili wa mezi Januari wakati baadhi ya wachezaji wakihusihwa na kusepa klabuni hapo.. Hata hivyo, Mourinho anaweka wazi kuwa klabu hiyo itakua na changamoto wakati wa kujihusisha na soko la wachezaji mwezi Januari.
Mourinho anasema klabu hii haitaweza kupambana na vilabu vingine vikubwa vya EPL kutokana na hali halisi ya klabu na mfuko wao. Kuna hofu kuwa wanaweza kuwapoteza wachezaji kadhaa watakaohitaji kuondoka lakini meneja huyu anasema inawapasa kujiandaa kuendana na hali hiyo kama klabu.
“Niko Tottenham Hotspur. Natambua wasifu wa klabu, natambua kazi iliyopo, natambua matazamio ya klabu, najua malengo. Natambua katika soko la uhamisho tunaenda kupambana na mabvo yanayoweza kutokea. Kama nilivyosema, baaadhi ya wachezaji wakiondoka tunatakiwa kuendana na hilo.” -Jose Mourinho
Mourinho amesisitiza kuwa anawapenda wachezaji alio nao, na kadri anavyoendelea kufanya nao kazi ndivyo anavyowafahamu zaidi. Ni matarajio yake kuwa atafanya vyema kuboresha ushambuliaji na ulinzi kwa wachezaji alio nao.
Povel
Duh. Ngoj tuone kwanza