Ndani ya dimba la Stade de France ambako mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya ulipofanyika jijini Paris nchini Ufaransa kumetokea simtofahamu baada ya video zilizokuwepo uwanjani kurekodia matukio kufutwa, huku mpaka sasa bado majibu ya kufutwa kwa yakiwa hayaridhishi.

Nje ya Uwanja wa Stade de France kwenye geti la kuingilia mashabiki wa Liverpool kulitokea vurugu ambazo zilisababishwa na kuwepo kwa tiketi bandia ambazo baadhi ya mashabiki waliuziwa, kushindwa kuoneka kwenye mifumo tambuzi ya kuingilia uwanjani na kusabisha polisi kutumia nguvu kuwatanya na kuwamwagia vipurizi vya kutoa machozi.

Stade de France
Stade de France

Ushahidi wa “CCTV” ulitosha kutumika kujua nini chanzo zha vurugu kwenye geti hilo, ambapo kwa sehemu kubwa mashabiki wa klabu ya Liverpool wamekuwa wakitupiwa lawama kwa kufanya fujo.

Erwan Le Prevost, mkurugenzi wa uhusiano wa kimataifa kwenye shirikisho la soka la Ufaransa alimwambia Senate kwamba Video za CCTV za uwanjani ‘automatically’ zimefutika baada ya siku saba.

“Ushaidi wa video unahifdhiwa ndani ya siku saba, baada ya hapo zinafutika kweny mfumo wa uhifadhi.” Alisema Erwan Le Prevost

Kutokupatikana kwa Ushaidi wa Video za uwanjani kunaleta uwalakini wa maamuzi ya uchunguzi kuhusu tukio zima la vurugu, Huku waziri wa michezo akiwa bado anawashutumu mashabiki wa Liverpool kuwa wao ndio chanzo cha fujo.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa