Wachezaji wawili wa klabu ya Chelsea ambao walikua majeruhi Raheem Sterling na Enzo Fernandez wameripotiwa kurejea mazoezini kuelekea mchezo wao wa nusu fainali wa kombe la Fa dhidi ya Man City.
Raheem Sterling aliripotiwa kuumia wiki kadhaa nyuma kama ilivyo kwa kiungo Enzo Fernandez, Lakini mapema leo wameonekana mazoezini na kikosi cha Chelsea kuelekea mchezo dhidi ya Man City utakaopigwa kesho.Klabu ya Chelsea imekua ikiandamwa na majeraha mara kwa mara msimu huu na idadi kubwa ya wachezaji kubwa ya wachezaji wa klabu hiyo wamepata majeraha jambo ambalo limechangia kudhorota kwa klabu hiyo.
Kurejea kwa Enzo na Sterling ni jambo kubwa kwa kikosi cha Chelsea kwani wamekua wachezaji muhimu ndani ya timu hiyo msimu huu, Lakini pia ukizingatia mchezo wa kesho ambao ni mgumu dhidi ya Man City.Klabu ya Chelsea na Man City msimu huu wamekutana katika michezo miwili ya ligi kuu ya Uingereza na yote miwili imemalizika kwa sare, Hivo kesho kenye nusu fainali ya kombe la Fa inasubiriwa kuona kama wataendelea walipoishia au mmoja atakubali kichapo.