Manchester City wameripotiwa kuwa tayari kumtoa Raheem Sterling na Gabriel Jesus kwa Tottenham Hotspur kwa ajili ya mshambuliaji nyota Harry Kane.

Baada ya kuchapwa kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa, City wanahusishwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa England msimu huu wa joto wakati wanaimarisha safu yao ya ushambuliaji.

Spurs wanasita kumuuza mchezaji huyu akiwa amebakiza miaka mitatu kwenye mkataba wake, haswa kumuuza kwa hasimu wao wa moja kwa moja wa Ligi Kuu.

Sterling na Jesus Karata ya Kumleta Kane City

Kwa mujibu wa The Sun, City wanaamini kwamba wanaweza kuwashawishi Tottenham kufanya biashara kwa kutoa washambuliaji kadhaa ili kupunguza athari ya kumpoteza Kane kwa Spurs.

Hata kama Spurs wangependa kumsaini Sterling na Jesus, City bado italazimika kulipa pesa kibao.

Jesus alifunga mabao tisa na kutoa usaidizi kwenye mengine manne katika Ligi ya Premia mnamo msimu wa 2020-21, wakati Sterling alihusika moja kwa moja katika mabao 17 katika msimu uliokwisha.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa