Steven Gerrard: Mwili wake ni Sehemu ya Liverpool

“Kuwa Legend wa timu haimaanishi kuwa unafaa kuwa Kocha wa timu hiyo” ni maneno ya Kocha wa Rangers ya Scotland, Steven Gerrard

Niliyatafsiri maneno yake kwa busara yake ya siku zote, nikikumbuka Fainali ya Liverpool dhidi ya AC Milan pale Istanbul 2005 Liverpool ilimuamini ingali mdogo kuvaa kitambaa cha Unahodha wakitwaa kombe lile.

Haikuwa issue sana, nikaikumbuka tena Jumapili baada ya Fainali nyingine ya Ulaya Liverpool vs AC Milan 2007, baada ya Liverpool kupoteza na Milan ikiwa moto wa kuotea mbali wakati huo.

Ule Usiku Kocha wa Milan Carlo Ancelotti alimfuata Kiungo wake Andrea Pirlo na kumwambia nataka nikuletee Steven Gerrard mcheze wote kwenye Kiungo, Pirlo alifurahishwa sana na akamwambia Carlo amletee kwa haraka sana

Sasa Jumapili baada ya ile fainali Carlo aliongea na Gerrard, jibu pekee alilopewa ni NO, Steve Gerrerd akiamini mwili wake ni kwa ajili tu ya uzi wa Liverpool na watu wa Liverpool, alikataa kwa zaidi ya wiki nzima ofa ya kwenda Milan licha ya kuwa ni mabingwa wa Ulaya

Pirlo baada ya muda mrefu kupita akamuuliza Kocha wake King Carlo, kwa huzuni sana Carlo alimjibu “Andrea ile ndoto yako ya kucheza nae haiwezi kutimia, nimejaribu kila namna ila amekataa, hayupo tayari kuachana na Liverpool”

Ikawa hivyo miaka yote Roman Abramovich alivyopeleka pesa kwa ajili yake akasema hapana, ikawa hivyo Perez wa Real Madrid alivyopeleka pesa akasema Hapana, yeye hakuamini maisha nje ya Liverpool pale Ulaya

Na huyo ndio Steven Gerrard, binadamu muungwana sana anaeamini Liverpool ni sehemu ya mwili wake


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

15 Komentara

    Steven alikuwa na mapenzi na Liverpool

    Jibu

    Good New

    Jibu

    Nikweli kabisa

    Jibu

    Hana mapenzi Sana na timu yake

    Jibu

    Steven anamapenz ya dhati na liverpool

    Jibu

    Duuh ila nikweli

    Jibu

    Safi

    Jibu

    😍

    Jibu

    Gerrad ameweka rekod kubwa anfield

    Jibu

    Gerrard ni mchezaji aliyejiwekea rekodi nzuri sana ndani ya Liverpool

    Jibu

    Gerrard alikuwa mtu mmoja hatari sana na kuweka rekodi nzuri

    Jibu

    Kweli

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Gerrard alikuwa mtu hatar sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet

Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.