Vyanzo mbalimbali vimethibitisha kuwa John Stones amekubaliana na Inter Milan kuhusu mkataba wa miaka miwili, ambao utamuingizia mshahara wa euro milioni 4 kwa msimu.

Hata hivyo, pamoja na makubaliano hayo na Stones, Inter haijaachana na mpango wake wa kumsajili beki wa Tottenham Hotspur, Cristian Romero. Klabu hiyo ya Serie A bado inamwona Romero kuwa moja ya malengo yake muhimu ya kuimarisha safu ya ulinzi.
Hii inaonyesha kuwa Inter inalenga kuongeza ubora na uzoefu katika eneo la ulinzi kwa kusajili zaidi ya beki mmoja, huku ikitarajia kumaliza dirisha la usajili ikiwa na safu ya nyuma yenye ushindani mkubwa.
Sky Sport Italia iliripoti mchana wa leo kuwa makubaliano ya awali kwa njia ya mazungumzo yamefikiwa kwa John Stones kujiunga na Inter Milan kama mchezaji huru, baada ya mkataba wake na Manchester City kumalizika bila kuongezwa.
Baadaye, vyanzo vingine kadhaa vilithibitisha taarifa hiyo, vikieleza kuwa makubaliano hayo yanahusisha mkataba utakaodumu hadi Juni 2028, huku Stones akitarajiwa kulipwa mshahara wa euro milioni 4 kwa msimu baada ya makato ya kodi (net).
Kwa kuwa Uingereza ilifika hadi hatua ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia, John Stones bado yupo mapumzikoni na hana haraka ya kufanyiwa vipimo vya afya. Kutokana na hali hiyo, tarehe ya vipimo hivyo bado haijapangwa.

Wakati huohuo, inafaa kufahamu kwamba Inter Milan inatafuta kusajili zaidi ya beki mmoja wa kati, baada ya Francesco Acerbi na Matteo Darmian kuondoka klabuni kama wachezaji huru katika dirisha hili la usajili.
Hii ina maana kwamba Inter Milan inaendelea na jitihada za kumsajili nyota wa Tottenham Hotspur, Cristian “Cuti” Romero, huku ikijaribu kufikia makubaliano na klabu hiyo kwa ada ya euro milioni 40.
Beki huyo wa kimataifa wa Argentina anaripotiwa kuwa na hamu ya kurejea Serie A baada ya uzoefu wake wa awali akiwa na Genoa, Juventus na Atalanta.


