Mshambulizi wa Atletico Madrid Luis Suarez anaripotiwa kutaka kuungana tena na Steven Gerrard huko Aston Villa.
Suarez aliisaidia Atletico kushinda taji la La Liga msimu uliopita, kampeni hii imekuwa na mafanikio duni kwa Staa huyu wa Uruguay akichangia mabao nane pekee kati ya mechi 26 alizocheza.
Huku ikiwa imesalia chini ya miezi sita kwenye mkataba wake, Suarez yuko kwenye nafasi ambayo anaweza kufanya mazungumzo na klabu za nje, lakini inaonekana ana mwelekeo wa kurejea Ligi Kuu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Uhispania Gerard Romero, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 yuko tayari kukataa ofa kutoka kwa vilabu kadhaa vya Brazil ili kuhamia Villa Park.
Ripoti hiyo inadokeza kuwa Gerrard tayari ameashiria nia yake ya kumleta mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool West Midlands.
Wawili hao walifanya kazi pamoja kati ya Januari 2011 na Julai 2014, na makubaliano yoyote yatafuatia Gerrard kuwa tayari anafahamiana na Philippe Coutinho kutoka Barcelona.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA