Mchezaji wa Atletico Madrid Luis Suarez anataka aliyekuwa kocha wa zamani Ronald Koeman amwambie kwanini alimuondoa katika klabu yake ya Barcelona miaka miwili iliyopita.
Suarez alijiunga na wapinzani wao ambao ni Atletico Madrid kwa uhamisho wa bure Septemba 2020 baada ya kuonekana kuwa ni mchezaji ambae alikuwa sio chaguo la kwanza katika kikosi cha Koeman. Msimu wa kwanza tu aliposajiliwa na timu ya Simeone akabeba na taji la Laliga.
Mshambulizi huyo wa Uruguay, alifunga mabao 198 katika kipindi cha miaka sita kilichobeba taji akiwa na Barca. Suarez anatumaini kuwa kocha huyo ambaye nae alitimuliwa na Wacatalunya hao Oktoba 2021 baada ya miezi 14 tu kama kocha mkuu, ataeleza kwa nini aliamua kuachana naye.
Aliiambia Marca: “Muda unasonga, na ndio, kwa ustaarabu na heshima zote , ningemsalimia.
Anaendelea kusema kuwa angekutana nae, antumaini kuwa angekuwa na ukubwa aliokuwa nao kama mchezaji katika klabu, angempa sababu za yeye kumuondoa kikosini hapo.
Xavi alichukua nafasi ya Koeman na ameungwa mkono kwa kiasi kikubwa katika dirisha la uhamisho na kuwasajili wachezaji walioleta matokeo chanya klabuni hapo akiwepo Roberto Lewndowski, Raphina, Jules Kounde na wengine wengi.
Mshambuliaji huyo wa Atletico anahisi kuwa gwiji huyo wa Barca Xhavi ana kila kitu kwasasa kitakachomfanya apate mafanikio na alipoulizwa ni kocha mzuri kwa Barcelona alisema; “Nafikiri hivyo, na anaonyesha bila kuwa mkamilifu. Ni kocha aliyekulia huko na anajua klabu na mshabiki wanahitaji nini.
Suarez anahisi gwiji wa Barca Xavi ana kila kitu ili kuwa na mafanikio.
Alipoulizwa iwapo Xhavi atatoa staili ya mashabiki wa soka ya wababe hao wa Catalunya, alisema: “Nafikiri hivyo. Anaonyesha hivyo, bila kuwa mkamilifu. Ni kocha aliyekulia huko na anajua klabu na mashabiki wanahitaji nini”.