Sven Akosha na Ajibu na Ndemla

Mbeligiji Sven Vandenbroeck, amefunguka kuwa amekoshwa na viungo wake Ibrahim Ajibu, Hassan Dilunga na Said Ndemla ambao walifunga mabao kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui FC kwa kubainisha wazi hiyo inaonyesha hamtegemei mtu mmoja kwenye suala la kufunga.

Mbelgiji huyo ameongeza kuwa mabao ya viungo hao yanamfanya sasa kuona timu yake ina uwezo wa kupata pointi kwa kufunga bila ya kuwategemea washambuliaji wao ambao walikosekana kwenye mechi kadhaa nyuma kutokana na majeraha.

Ajibu, Dilunga na Ndemla walifunga mabao wakati Simba ikishinda mechi yake ya ligi kuu mbele ya Mwadui FC kwa mabao 5-0 katika Uwanja wa Uhuru, Oktoba 31. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na John Bocco aliyefunga mawili na Hassan Dilunga.

Sven amesema kuwa kitendo cha wachezaji hao kufunga kinampa wigo wa kuona wana uwezo wa kupata mabao na pointi kwenye mechi yoyote bila ya kuwategemea washambuliaji wake halisi ambao kwa sasa ni wagonjwa.

“Kila mmoja anaweza kufunga mabao hapa wala siyo kuwategemea Bocco, Kagere au Mugalu pekee. Ndemla, Dilunga wamefunga, ni jambo zuri na hii inafanya tuwe na mifumo mingi ya kucheza na tukapata mabao.

“Kocha anaweza kumpenda mshambuliaji anayefunga mabao 15 kwa msimu lakini siku ambayo akikamatwa na wapinzani timu haitafunga, hivyo kwa namna hii ya kila mtu kufunga inanifanya niwe na mbinu mbadala za kupata pointi,” alimaliza Mbelgiji huyo.


USHUJAA UNAKULIPA HAPA!

Hii ni halisi kwa ajili ya mashujaa wote! Ukiwa jasiri unavuna mkwanja kibao hapa na sloti hii ya Huangdi Casino. Waka nusu tukupe maradufu!

Ingia Mchezoni!

22 Komentara

    Simba wanaviungo wazuri sana

    Jibu

    Simba kwa sasa wako vizuri mashabiki tunafurahia

    Jibu

    Wote tunajua kuwa simba wanawachezaji vizuri ambao hawategemee mchezaji yoyote kwenye timu yao

    Jibu

    Simba wapo vzr sana

    Jibu

    Safi sana mpaka kocha kasema hivyo ujue amewaelewa

    Jibu

    Ha ha ha simba bwanaa

    Jibu

    Hao ndo simba hawana kazi mbovu

    Jibu

    Kweli kabisa yupo sahii ndiocho kitu kinacho takiwa kutomtegemea mtu kufunga kwasababu mtu yoyote akiwa amekaa vizuri nagoli lazima afunge nasio kumtegemea mtu kwenye mechi mfungaji malufu ndio afunge inakuwa siopoa kwai akitoke yulemfungaji Kama ayupo kwai magoli ayafungwi lakini kwasimba tunaviungo makini Sana nawafungaji Kama ote naikubali Sana simba

    Jibu

    Kumbe

    Jibu

    Ila kikosi cha simba kipo imara mambo yote tarehe7 pale kwa mkapa

    Jibu

    Simba kuna majembe

    Jibu

    Simba bigwaa

    Jibu

    Simbaaaaaa wako vizuri sana

    Jibu

    Imeisha hiyoooo

    Jibu

    Simba wapo vizuri sana

    Jibu

    Simba baba lao uwa hatunag maneno mengi sie!

    Jibu

    Ibrahim hana maajabu yoyote

    Jibu

    Simba imara

    Jibu

    Hao watu ni nomaa

    Jibu

    Asiw na presha angoje kipigo tu kweny kkoo derby

    Jibu

    Mambo ni moto kuelekeah Kariakoo DERBY

    Jibu

    Huyu Seven dawa yake ipo jikon

    Jibu

Acha ujumbe