Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kuwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City anaweza kumpa nafasi mshambuliaji wake Chris Mugalu ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha.

Leo Desemba 13, Simba inakibarua cha kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City inayopambana kujinasua kutoka kwenye mstari wa kushuka Daraja.

Ikiwa imecheza mechi 14 imekusanya pointi 12 na inashika nafasi ya 15 inakutana na Simba iliyo nafasi ya tatu na pointi 26 baada ya kucheza mechi 12.

Sven, Sven Kuivaa Mbeya City Full Mkoko, Meridianbet

Sven amesema :-“Tumekuja na wachezaji 21 na wote wapo tayari kwa mchezo wetu. Mbeya City ni timu hatari, hawajapoteza kwenye michezo mitano iliyopita hivyo lazima tuwe vizuri zaidi ili tuweze kuibuka na ushindi.

“Nategemea kumtumia Mugalu kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ninadhani anaweza kuanza benchi kisha nitampa nafasi ya kucheza ili ajenge hali ya kujiamini,” amesema.

Sven, Sven Kuivaa Mbeya City Full Mkoko, Meridianbet

Kwenye Ligi Kuu Bara, Mugalu ametupia jumla ya mabao matatu kati ya 31 ambayo yamefungwa na Simba kwa msimu wa 2020/21.


MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

Sven, Sven Kuivaa Mbeya City Full Mkoko, Meridianbet

SOMA ZAIDI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa