Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji amecharuka na kuwataka wachezaji wake kucheza kwa kujituma kuelekea kwenye mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.
Simba ilipoteza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Platinum uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kwa kufungwa bao 1-0 lililopachikwa na Perfeck Chikwende.

Ina kibarua cha kupindua meza Uwanja wa Mkapa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Januari 6, ambapo Ofisa Habari wa timu hiyo Haji Manara amesema kuwa utakuwa ni mchezo wa vita ndani ya Dar.
Vandenbroeck amesema kuwa kilichowaponza washindwe kushinda mchezo huo ni kukosekana kwa umakini kwa wachezaji wake jambo ambalo limemkasirisha hasa hivyo hatapenda kuona makosa yanajirudia.

“Tuliweka wazi malengo yetu tangu awali kwamba ni lazima tuweze kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Kuanza kwa kupoteza hiyo ni mbaya kwetu na haijanifurahisha hasa kwa kuwa mchezo tuliweza kuumiliki ila umakini ulikosekana.
“Kwenye mchezo wetu wa marudio hatuna chaguo la kufanya zaidi ya kutafuta matokeo chanya na wachezaji kujituma zaidi, hivyo mashabiki watupe sapoti tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema Vandenbr.oeck.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?




Dorophina
Simba washaanza kuwa mdebwedo
Saupha mohamed
Simba inazingua sana
Lydia Emmanuel Magoti
Kweli yupo sahii
Fatina mfingi
Simba mbona kma mmeanz kutukosesha raha!!
Mwanahamisi
Simba inazingua kinoma
Asia Abdy
Wakazee
Issa
Makini sana
warda
Bila kujituma huwezi fanikiwa
Tatu
Wakaze tupate ushindi
Sarah
Nikweli simba wajitume ili wampate ushindi
Hopemwaikuka
Kabsaa wakaze
Angelina
Yuko sahihi
Shakila mrope
Yuko makini san
Zahara omary
Yupo makini sanaa kiukweli
Sania
Kujituma ni muhimu sana katika soka kwahiyo simba wasijibweteke