Chris Hughton ndiye anayetazamiwa kuwa mshindani mkubwa katika nafasi ya kukinoa kikosi cha Watford mara baada ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho kuondolewa kutokana na matokeo mabovu ya kikosi hicho. Kocha huyo huenda akafikiriwa zaidi kupewa mikoba hiyo baada ya kupigiwa upatu zaidi na safu ya uongozi wa klabu hiyo kwa kuonekana anaweza kuwa na falsafa za klabu hiyo.

Nyota wa zamani wa Arsenal amefutilia mbali tetesi zinazodai kwamba huenda akaachana na kazi ya kufundisha kikosi cha Nice baada ya kuanza kuhusishwa na kujiunga na klabu yake ya zamani kama mkufunzi atakayeshika nafasi ya Emery ambaye aliondoshwa na klabu hiyo kutokana na kushindwa kuendana na malengo ambayo klabu ilijiwekea.

Aliyekuwa kocha wa Tottenham anaviziwa kuanza kuhusishwa kujiunga na klabu za Manchester United na Arsenal. Klabu hizo zipo katika hatihati ya kuangalia utawala mpya ambao unaweza kuwa na matokeo yanayoridhisha mbali na ilivyo hivi sasa kwa klabu hizo. United wao wapo katika hatua za kukisuka kikosi chao na huenda wakahitaji mtu ambaye ataleta mabadiliko ya haraka sana kikosini hapo.

Jose Mourinho, kabla ya kuchukua jukumu jipya la kukinoa kikosi cha Spurs, inasemekana alikuwa tayari ameahidiwa kiwango fulani na klabu ya Real Madrid ili asipokee kazi ya aina yoyote na asubiri hadi pale klabu hiyo itakapomtimua Zidane. Klabu hiyo ya Spurs, kutokana na kuwa bado na mkataba na kocha huyo, ililazimika kuanza kufanya mazungumzo ya kumnasa kabla hawajawahiwa na klabu hiyo.

Huenda nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya klabu ya Lyon akarudi ndani ya taifa hilo la Uingereza lakini katika klabu tofauti na ile aliyotoa huduma yake kipindi alipokuwa ndani ya taifa hilo. Depay ananyemelewa na klabu za Liverpool na Spurs ambao wamevutiwa na nyota huyo kwa mara nyingine ili arejee ndani ya taifa hilo.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa