Kumezuka mjadala mkubwa juu ya miamba miwili ya kati, Mukoko wa Young Africans na Lwanga wa Simba, ni yupi bora Kati yao? Ni yupi anaweza kumweka bench mwenzie wakiwa timu moja?

Kwa elimu yangu ndogo sana, nachofahamu mpira wa miguu una kitu kinaitwa ROLE AND POSITION, yani nafasi na majukumu, nafasi ya wachezaji inaweza kufanana ila majukumu yakawa tofauti, huo ndio mpira ulivyo

Taddeo Lwanga ndani ya Simba ni kama Sergio Busquets ndani ya Barcelona au Ngolo Kante wa msimu wa kwanza pale Chelsea, nafasi yao ilikuwa ni namba sita ila majukumu yakiwa ni kukaba zaidi (Holding role)

Lwanga, Taddeo Lwanga Vs Mukoko Tonombe, Meridianbet

Juu ya Lwanga kuna Rally Bwalya, Clatous Chama na Luis Miquissone, juu ya Busquets kulikuwa na Iniesta,Xavi na Messi, juu ya Kante kulikuwa na Fabregas, point yangu hapa ni kuwa kazi ya Lwanga, Busquets na Kante ni Blocking, interception na kulinda back four, kupora mpira kisha waachie viungo wacheze.

Lwanga, Taddeo Lwanga Vs Mukoko Tonombe, Meridianbet

Lwanga anashindanishwa na Mukoko kwakuwa anafunga na kuonekana zaidi ila narudia tena kuna NAFASI NA MAJUKUMU, Lwanga analinda umbo la Simba, analazimika kucheza eneo la chini zaidi kuilinda timu kwenye counter na halfspaces ile nafasi isipatikane kisha mpira uende eneo la juu yake hapo ndipo unapikwa sasa (creative hub).

Lwanga, Taddeo Lwanga Vs Mukoko Tonombe, Meridianbet

Mukoko yupoje ndani ya YANGA? Kwa nafasi ya Mukoko ni kama Lwanga ila kwenye majukumu ndipo utofauti wao unakuja, kwanza akiwa na deeper role anaufuma mchezo kutokea chini ni Regista role, lakini bado ni kama Box to box, hapa anabadilika kabisa na kuwa kama Vidal au Gerrard.

Mukoko anayafanya yote haya kutokana na timu anayocheza kwasasa, inamlazimu mwalimu amtumie kama Prober kwakuwa hana mtu mwingine, kuna muda analazimika kumtumia kama Ball carrier kwakuwa hana mwingine na kuna muda anasimama kama holder, vyote anaweza kukupa kwa mechi moja tu, kwanini? Ni kutokana na quality ya wachezaji waliopo

Lwanga, Taddeo Lwanga Vs Mukoko Tonombe, Meridianbet

Je ni nani bora kati ya LWANGA na MUKOKO? Kwangu mimi wote ni bora kwakuwa Mchezaji bora ni yule anaetumwa majukumu na kufanya majukumu yake kama ambavyo ametumwa na Mwalimu, LWANGA anatimiza kwa 100% na MUKOKO anatimiza kwa 100%


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

Lwanga, Taddeo Lwanga Vs Mukoko Tonombe, Meridianbet

  CHEZA HAPA

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa