Nililazimika kuusubiri usiku wa saa nane ili niweze kutafakari kwa utulivu zaidi, nililazimika kuusubiri mchana wa saa nane ili nipate wasaa wa kuandika vema zaidi, Nililazimika kuisubiri jioni ya saa kumi niweze kuachilia hili andiko.

Si shairi la mahaba, la! Si muendelezo wa makala niliyoipotezea siku za nyuma, la! Si sehemu ya riwaya yangu ya Nisamehe dunia, la! Si maoni yangu juu ya mabao manne ya Olivier Giroud usiku wa jana, la! Ni juu ya mganda aliyetua Unyamani, Taddeo Lwanga.

Taarifa kutoka kwa vyanzo ninavoviamini vinadai, Taddeo alivunja mkataba na klabu yake ya Misri, walishindwa kumlipa mshahara kwa muda mrefu. Na si alitemwa kama inavodaiwa, si alifeli kama inavodaiwa. Maslahi bwana! Nipe muda kidogo nikuambie kitu kumuhusu Claudie Makelele.

Mwaka 2003, Real Madrid iliyosheheni Galacticos ilitwaa la liga. Ndani ya kikosi alikuwepo Claudie Makelele. Msimu ulipoisha alimfuata rais Florentino Perez ofisini na kumuambia, kocha Vicente del Bosque ameniambia bado ananihitaji kwa muda mrefu, tunaweza kujadili mkataba mpya?

Perez alitabasamu akamuambia, “tutakupa mkataba mpya, japo hautafanana na Zidane lakini utakuwa mnono zaidi ya huu wa sasa”. Makelele hakujalisha, alichoridhika ni kwamba atabaki Real Madrid kwa maslahi zaidi. Perez akampa mkono akamuambia, nenda ukafurahie likizo yako.

Lwanga, Tadeo Lwanga Katika Fikra za Claudie Makelele, Meridianbet

Makelele alirejea kutoka likizo akijua ana miaka minne zaidi Madrid, lakini haikuwa hivo. Perez alimuambia klabu imetumia pesa nyingi kumsajili David Beckham, hivo hamna pesa ya kumlipa, kama Makelele anataka asaini mkataba bure kwa sababu Real Madrid ni timu ya ndoto ya kila mchezaji.

Makelele alikataa akaamua kujiunga na Chelsea, kwake mpira haukuwa burudani, mpira ulikuwa kazi, mpira ulikuwa baba na mama kwake. Kivipi asaini mkataba wa bure kisa ya mafanikio ya jina? Alienda Chelsea na mpaka leo wanakiri London Magharibi hawajawahi kumuona kiungo mkabaji kama Claudie. Ameshinda mataji kibao pale, ana heshima kubwa sana pale.

Lwanga, Tadeo Lwanga Katika Fikra za Claudie Makelele, Meridianbet

Itazame tena picha ya Taddeo kisha uniulize, kwanini ameondoka Misri? Nitakuambia amefuata njia ya Claudie Makelele. Maslahi bwana!


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Lwanga, Tadeo Lwanga Katika Fikra za Claudie Makelele, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

22 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa