Taffarel Ajiunga na Benchi la Ufundi Liverpool.

 

Golikipa wa zamani wa Brazil na mshindi wa kombe la Dunia Claudio Taffarel, 55 amejiunga na benchi la makocha (ufundi) katika klabu ya Liverpool.

Kipa huyo wa zamani wa Brazil amabae alishinda Kombe la Dunia mwaka 1994 atajiunga na John Achterberg na Jack Robinson kuwa makocha wa magolikipa katika klabu ya Liverpool.

Taffarel atafanya kazi katika klabu ya Liverpool lakini vile vile ataendelea kuwa kocha wa makipa katika timu ya Taifa ya Brazil.

“Tuliongea na Ali [Becker] kwasababu makipa bora duniani ni wabrazil na tulipata suluhisho la kumleta Taffarel na umekuwa mchango mkubwa kwenye benchi la ufundi,” alisema Meneja Jurgen Klopp

 

“Tunafikiri inaweza kutupa mtazamo tofauti tena, kuangalia vitu tofauti.

 

“Tunataka kuwa shule iliyokamilika ya magolikipa katika dunia ya mpira na ndomaan atumemleta mwalimu wa tatu wa makocha ambaye ana uzoefu mkubwa, mkubwa sana.” aliongeza.

 

Becker and Taffarel

 

 

 

 


MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe