UONGOZI wa kikosi cha Taifa Stars umeweka wazi kuwa unaendelea vizuri na maandalizi ya kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani yaani Chan dhidi ya Somalia, huku wakiweka wazi kuwa wana matumaini makubwa ya kufuzu mashindano hayo.

 

Taifa Stars, Taifa Stars ina Matumaini ya Kutoboa CHAN., Meridianbet

Taifa Stars inatarajiwa kuvaana na Somalia katika michezo miwili ya kusaka kufuzu Chan ambapo mchezo wa kwanza utapigwa Julai 23 na wa pili ukipigwa Julai 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kuelekea michezo hiyo Stars jana Jumamosi iliendelea na mazoezi ya kujiandaa na michezo hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema: “Wachezaji wote waliojumuishwa kwenye kikosi wanaendelea na mazoezi kuelekea michezo hiyo miwili, isipokuwa baadhi ambao wana sababu mbalimbali.

 

“Kwetu matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa kwa kuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunakata tiketi ya kufuzu mashindano haya.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa