Serikali ya Tanzania, kupitia Waziri Mkuu limeiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwasilisha taarifa ya sakata dabi ya watani wa jadi ambayo ilipaswa kufanyia tarehe 8 Mei 2021 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Jijini Dar es Salaam.
Dabi hii ya watani, Simba na Yanga, imetawala na sarakasi kadhaa juu ya masuala ya kiutaratibu na suala zima la kufuata maelekezo.
Kumekuwa na mgawanyiko kati ya wale wanaosimamia kanuni za ligi, na wale wanaoona ilikuwa sawa ikiwa timu zingekubaliana na mabadiliko yaliyofanyika, licha ya kukiuka kanuni.
Hata hivyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kipindi cha utambulisho wa wageni Bungeni, ameagiza wizara husika kuwasilisha taarifa kamili ya kilichotokea na hatma kwa ya sakata hilo kwa kuzingatia wanaanchi pia ambao tayari walilipa fedha na kupoteza mda wa maandalizi kwa ajili ya mechi ambayo baadaye ikaahirishwa.
“Kufuatia kero hii tayari tumeagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha inatoa taarifa haraka sana kwa Watanzania, mchezo wenyewe utachezwa lini lakini kuna viingilio ambavyo walikuwa wametoa mashabiki hatima yake nini”
Naomba kuwasihi Watanzania hasa wapenzi wa michezo kwenye eneo la mpira wa miguu ambao walijiandaa kusikia na kuangalia mpira wa miguu, tuipe muda wizara itoe taarifa kwa kushirikiana na taasisi inayoshughulikia mpira wa miguu,” .
-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Sakata hili limegusa hisia za mashabiki wengi wa mchezo huu, ambao wamelipa pesa na kutenga muda kwa ajili ya kuhudhuria moja ya mechi yenye historia kubwa.
Baadhi ya wapenzi wa pambano hili la watani wa jadi walitoka nchi zingine. Bila shaka Wizara kwa kushirikiana na TFF, watafikia muafaka wenye manufaa kwa pande zinazohusika.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Ila sio poa
Soka letu sijui litakua lini hadi selikali iingilie kati
Kweli kabisa utuambie sababu za muhimu
Mambo ya soka bhana!!!
Sio poa kabisa
Kosa la TFF sisi yanga tuliondoka zetu
Walichokifanya sio kizuri kwa mashabiki
Duuh sio poa
Kwakweli siku ya tarehe8 mashabiki turibaki njia panda hatufurahia uamuzi wa kuairisha mechi
Duuh kaz ipo hapa
Safi Sana wazir
Hawakufanya poa
Safi sana