Klabu ya West Ham itajaribu kumsajili nyota wa Chelsea, Tammy Abraham kwa mkopo kwenye dirisha kubwa la usajili linalokuja mara baada ya Chelsea kuweka dau la paundi milioni 40 kama thamani ya nyota huyo.

Dau hilo linatajwa kuzifukuza timu kadhaa zinazoonyesha nia ya kutaka kumsajili jumla zikiwemo klabu za Aston Villa, Newcastle na Leicester city hivyo West Ham imeona njia rahisi kumpata mshambuliaji huyo ni kwa kumtaka kwa mkopo.
Inataarifiwa kwamba kuna uwezekano mshambuliaji huyo akaomba kuondoka mara baada ya kukosa nafasi ndani ya kikosi cha Chelsea chini ya kocha Thomas Tuchel.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Duuh mambo hayo
Kama amekubari kwenda huko kwa mkopo sawa ila siyo poa
Hongera sana Tammy kazi popote
Hongera sana Tammy
Hongera
Safii