Kocha wa klabu ya Manchester United Eric ten Haag amesema anataka kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora wake ambao imekua na kwa miaka mingi, amezungumza hayo kuelekea mchezo wao dhidi ya Aston Villa katika michuano ya Carabao Cup.

Kocha huyo amesema anapanga kuirudisha klabu hiyo katika zama zake za ubora ambazo klabu hiyo ilikua ikifanya vizuri kwa kiwango kikubwa na kuifanya timu hiyo kua tishio zaidi duniani.ten haagKlabu ya Manchester United imekua haifanyi vizuri tangu kuondoka kwa kocha gwiji wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson ambae aliipata mataji mengi klabu hiyo kipindi cha utawala wake na kuifanya klabu hiyo kua tishio zaidi duniani.

Tangu kuondoka kwa Ferguson mwaka 2013 klabu hiyo imefanikiwa kubeba mataji matatu tu huku wakipita makocha takribani matano huku wakishindwa kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora.

Lakini Ten Haag yeye anaamini anaweza kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora wake ambao ilikua nao kipindi cha Sir Alex Ferguson ambapo klabu hiyo ilikua ni miongoni mwa timu za kuogopwa zaidi sio tu Uingereza bali duniani kwa ujumla.ten haagMashabiki wengi pia wa klabu hiyo wanaamini Ten Haag anatakiwa kupewa mda ili aweze kutengeneza timu yake na kuifanya kua tishio huku wakitoa mifano kwa makocha kama Jurgen Klopp, na Mikel Arteta ambao vilabu vyao viliwapa muda na matunda yakaonekana.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa