Kocha wa klabu ya Manchester United Eric Ten Haag amezungumza kuhusu nyota wa klabu hiyo kuomba msamaha baada ya kupewa adhabu siku kadhaa zilizopita.ten haagWiki kadhaa zilizopita staa wa klabu ya Mancherster United Cristiano Ronaldo alipewa adhabu na klabu hiyo, Baada ya kufanya kitendo cha utovu wa nidhamu katika mchezo dhidi ya Tottenham ambapo aliondoka kwenye benchi kabla ya mchezo kumalizika.

Kutokana na hali hiyo kocha huyo ameulizwa leo kabla ya mchezo wao na klabu ya West Ham kama staa huyo aliomba msamaha “Je Ronaldo aliomba msamaha? Inatosha kuzungumzia suala hilo, Nadhani nilishatoa maelezo ya Kutosha.  Tunafurahi kwakua yupo hapa na Cristiano ni Mchezaji mzuri” Ten haag alimalizia kwa kusema “Alhamisi alifunga bao tunafurahia hilo. Anaweza kuendelea kua muhimu zaidi.ten haagVijana wa Ten Haag leo watakua dimbani kumenyana na klabu ya West Ham wakiw katika dimba la Od Trafford huku wakitafuta mchezo wao wa nane bila kupoteza kwenye michuano yote. Ikumbukwe klabu hiyo imepoteza mchezo wake wa mwisho mwezi Oktoba mwaka huu dhidi ya Manchester City.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa