Kocha wa Manchester United Eric Ten Haag ameweka wazi anafikia kuingia sokoni na kutafuta beki mpya wa kulia kwajili ya kutoa ushindani wa namba kwa mabeki wa kulia waliopo klabuni hapo.

Ndani ya klabu ya Manchester United kuna mabeki wawili wa kulia lakini mmoja ndio anaonekana kufanya vizuri na kuimarika kwa kiwango, Na kocha wa klabu hiyo anatambua kuimarika kwa kiwango cha beki Diogo Dalot lakini anahitaji beki mwingine kwajili ya kuleta ushindani kikosini pamoja uwepo wa michuano mingi.ten haagBeki mwingine wa klabu hiyo Aaron Wan Bissaka anaonekana ni wazi hayupo kwenye mipango ya mwalimu Ten Haag kutokana na ufinyu wa nafasi ambao amekua akiupata klabuni hapo tangu kuwasili kwa mwalimu huyo majira ya joto.

Huku ikielezwa Man United wanatafuta namna ya kumalizana na Wan Bissaka ili kuachia nafasi ya kuweza kusajili beki mwingine wa kulia klabuni hapo.ten haagMwalimu Eric Ten Haag inaelezwa alivutiwa na beki wa Barcelona aliepo kwa mkopo klabu ya Ac Milan Sergino Dest katika majira ya joto lakini ndani ya dirisha dogo haiwezekani tena, Hivo inabidi kutafuta beki mwingine mbadala na kuweza kumsajili.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa