Kocha wa klabu ya Manchester United Ten Hag amechukizwa na kitendo cha mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno kwa kitendo chake cha kuondoka uwanjani kabla ya mchezo kuisha.

Cristiano Ronaldo baada ya kutokuwepo kwenye safari ya Pre-season na kukosa michezo dhidi ya Liverpool nchini Thailand ambapo United walishinda 4-0 na mchezo dhidi ya Atletico Madrid ambao walipoteza 0-1. Ronaldo alifannikiwa kuanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano kwenye uwanja Old Traford.

Ronaldo, Ten Hag Achukizwa na Ronaldo, Meridianbet

Kwenye mchezo dhidi ya Rayo Vallecano alifanikiwa kucheza kwa dakika 45 kabla ya kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Amad Diallo, Baada ya kutolewa Ronaldo aliondoka moja kwa moja kwenye viwanja hivyo kabla ya mchezo huo kuisha.

Kuna wengi waliondoka nyumbani, wala siwaraumu kwa hili, hii haikubaliki. Kwa yoyote. Nimewaambia kwamba haikubaliki. Sisi ndio timu, kikosi. Na unapaswa kubaki hadi mwisho,” alinukuliwa Ten Hag baada ya Ronaldo kuoandoka uwanjani.

Ronaldo mpaka sasa hatma yake haijurikani kwenye kikosi cha Man Utd kwani tayari alishawasirisha hati ya kuomba kuondoka kwenye klabu hiyo.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa