Ten Hag Aendelea Kumkopesha imani Antony

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag bado ameendelea kuamini kua mchezaji wake Antony Santos raia wa kimataifa wa Brazil anaweza kurejesha makali yake ambayo alikua nayo.

Winga Antony amekua hana wakati mzuri tangu ajiunge na klabu ya Manchester United akitokea klabu ya Ajax Amasterdam ambako aliwahi kufanya kazi na kocha Ten Hag na kuonesha ubora mkubwa.antonyKocha huyo amesema anaamini mchezaji huyo anaweza kurudisha makali yake ambayo alikua nayo, Kwani kocha huyo anasema Antony alikua moja ya wachezaji wasiozulika kirahisi na mwenye kasi haswa kwenye 10 yadi.

Winga huyo wa kimataifa wa Brazil licha ya kutokuonesha kiwango bora msimu ulioisha ndani ya klabu hiyo lakini alikua akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara, Lakini kwasasa imekua tofauti kwani amepoteza nafasi kabisa ndani ya kikosi cha mashetani wekundu.antonyPamoja na yote yanayotokea kwa winga Antony lakini bado kocha Erik Ten Hag anaamini mchezaji huyo atarejesha makali yake ambayo alikua nayo miaka miwili nyuma wakati wakifanya kazi kwa pamoja ndani ya kikosi chas Ajax nchini Uholanzi.

Acha ujumbe