Ten Hag Aendelea Kumkingia Kifua Rashford

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameendelea kumkingia kifua mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza ambaye amekua chini ya kiwango msimu huu.

Ten Hag anaamini Rashford atarejea kwenye ubora wake ambao alikua nao msimu uliomalizika, Kwani mchezaji huyo msimu huu ameonekana kuporomoka kiwango sana.ten hagMarcus Rashford msimu uliomalizika alifanikiwa kufunga mabao 30 kwenye michuano yote na kufanikiwa kuvunja rekodi ya Robin Van Persie iliyodumu klabu hapo kwa takribani miaka kumi, Hii ilitokana na ubora mkubwa aliokua nao mchezaji huyo ambapo msimu hajafanikiwa kuonesha ubora huo hata nusu.

Kocha Ten Hag ameeleza kua mchezaji huyo anapambana sana mazoezini kwajili ya kuhakikisha anarudisha ubora wake, Huku yeye akiamini atarejesha makali yake ambayo alikua nayo msimu uliopita kwa kufunga magoli yaliyoibeba timu hiyo.ten hagSafu ya ushambuliaji ya klabu ya Manchester United inaonekana kudorora sana kwasasa, Huku ikielezwa kushuka kwa kiwango Marcus Rashford pia kumechangia kwa kiwnago kikubwa kwani mchezaji huyo ndio alikua mfungaji bora klabuni hapo msimu uliomalizika.

Acha ujumbe