Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameendelea kumkingia kifua winga wake raia wa kimataifa wa Brazil Antony ambaye ameendelea kua chini ya kiwango ndani ya klabu hiyo.

Ten Hag amesema anaamini Antony bado ni mchezaji sahihi ndani ya klabu ya Manchester United, Kwani mchezaji huyo ana uwezo wa kupambana na ni shujaa hivo anaamini atafanikiwa kurudi kwenye ubora wake.ten hagKlabu ya Manchester United imekua kwenye mfululizo mbaya sana wa matokeo msimu huu na moja wa wachezaji ambao wanaonekana kua chini ya kiwango ni winga wa kimataifa wa Brazil Antony.

Kocha huyo anasema kwasasa timu nzima haicheza vizuri na sio Antony kitu ambacho yeye kama kocha wa timu anatakiwa kuwajibika, Lakini anaamini kua moja ya sababu za Antony kutokufanya vizuri ni timu pia kutokufanya vizuri.ten hagAntony ameanza kuzungumzwa kwa namna ya tofauti na mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kiwango chake ambacho kinaonekana kuporomoka kwa kiwango kikubwa, Lakini Ten Hag ni mtu ambaye anaamini mchezaji huyo anaweza kurejesha ubora wake.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa